Wanaume waliofumaniwa wakifanya mapenzi Indonesia wamechapwa viboko 85 kila mmoja

Wanaume waliofanya mapenzi wachapwa vikobo 85 Indonesia Haki miliki ya picha JUNAIDI
Image caption Wanaume waliofanya mapenzi wachapwa vikobo 85 Indonesia

Wanaume wawili wamechapwa viboko 85 kila mmoja kwenye mkoa wa Ace nchini Indonesia baada ya kufumaniwa wakifanya mapenzi.

Wanaume hao walisimama kwenye jukwaa wakiwa na mavazi meupe wakiomba, huku kundu la wanaume likiwachapa vikobo kwenye migongo yao

Indonesia imeharamisha mapenzi ya Jinsia moja na Mkoa wa Acheh hutawaliwa na sheria ya kidini- Sharia.

Adhabu hiyo ilitolewa mbele ya umma.

Wanaume hao wa miaka 20 na 23 walifumaniwa wakiwa ndani ya kitanda na makundi ya sungusungu yaliyovamia makaazi yao mwezi machi.

Kabla ya kufumaniwa na kundi la sungu sungu mmoja wao alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akisomea udaktari.

Image caption Adhabu hiyo ilitolewa nje wa msikiti kwenye mji wa Banda Aceh

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa mipango yake ilikuw akuwe daktari. Kwa sasa inaripotiwa kuwa chuo alichokuwa akisomea kimemtimua.

Video za wawili hao wakifumania zilisambazwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wote uchi huku wakiomba msaada.

Sheria kali dhidi ya mapenizi ya jinsia moja zilipitishwa mwaka 2014 na kuanza kutekelezwa mwaka uliofuatia.

Hukumu za kuchapwa viboko zimetolewa awali kwa makosa yanahusu kucheza kamari na unywaji pombe.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanaume hao wa miaka 20 na 23 walifumaniwa wakiwa ndani ya kitanda na makundi ya sungusungu yaliyovamia makaazi yao mwezi machi.

Mada zinazohusiana