Mwigizaji maarufu wa filamu za James Bond Roger Moore amefariki

Roger Moore amefariki baada ya kuugua saratani
Image caption Roger Moore amefariki baada ya kuugua saratani

Mwigizaji maarufu wa filamu za James Bond Roger Moore amefariki.

Katika taarifa ya familia yake marehemu iliochapishwa katika mtandao wake wa Twitter, walisema ''ni vigumu kutangaza kifo cha baba yetu Roger Moore ambaye amefariki nchini Switzerland baada ya kuugua saratani''.

Haki miliki ya picha iStock
Image caption James Bond

Roger Moore ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 89 alirahisisha kazi ya James Bond , jukumu ambalo lilimfanya kuwa maarufu sana.

Ilianza filamu ya Sean Connery ya 007 na baadaye sardonic humor ambayo ilizua hisia nyingi.

Aliwahi kuwa mwigizaji aliyeigiza kwa kipindi kirefu katika filamu ya James Bond huku filamu zake 7 za Bond zikiuzwa sana.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roger Moore katika filamu ya Persuader

Roger Moore alizaliwa mjini Stockwell kusini mwa mji wa Landon mnamo tarehe 14 Oktoba 1927 akiwa mwana wa afisa wa polisi.

Akiwa katika umri wa miaka 15 alienda chuo kikuu kabla ya kuwa mwanafunzi katika uhaishaji Studio ambapo alifurahia sana.

Umaarufu wa Sir Roger Moore uliimarika 1962 alipoigiza kama Simon Templar aka The saint katika kipindi cha runinga cha Leslie Charteries stories.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alirahisha jukumu la James Bond

Msururu huo wa kipindi ambao ulirekodiwa kwa miaka saba ulimfanya Roger Moore kuwa nyota pande zote mbili za Atlantic.

Tabia zake za kuweza kuingiliana na watu wengine, mzaha wake wa kuchezesha nyusi na uwezo wa kumfurahisha mwanamke yoyote yule zilishirikishwa katika jukumu lake la James Bond.

Roger Moore alifanikiwa sana katika filamu kama vile Shout at The Devil, The Wild Geese na North Sea Hijack, lakini taarifa nyingi za magazeti ziliangazia maisha yake ya nje baada ya kustaafu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aliendelea kujihusisha na James Bond hata baada ya kustaafu

Roger Moore alipona upasuaji wa saratani ya tezi dume 1993 na kusema kuwa alikuwa na bahati kubwa sana .

Alikuwa na nyumba nchini Switzerland na Monte Carlo ,lakini alitumia wakati wake mwingi akizuru maeneo tofauti ulimwenguni kama balozi wa Umoja Mataifa wa shirika la watoto Unicef.

Aliigiza filamu kama vile Octopussy, The Spy who Loved me, a View to A Kill na Live and let Die

Mada zinazohusiana