Maneno ya Kiswahili yaongezwa kamusi ya Kiingereza Kenya

Mwendeshaji pikipiki akiwa amembeba abiria Haki miliki ya picha AFP

Maneno kadha ya Kiswahili yameongezwa kwenye kamusi ya Kiingereza ambayo inakusudiwa kutumiwa na wanafunzi wa shule za msingi nchini Kenya.

Kamusi hiyo imechapishwa na matbaa ya Chuo Kikuu cha Oxford (OUP), na ni makala ya tatu.

Pia, kuna maneno yenye asili ya lugha nyingine za Afrika Mashariki au yaliyotoholewa na kuanza kutumiwa katika Kiswahili, ambayo yameongezwa kwenye kamusi hiyo.

Miongoni mwa maneno hayo ni:

Bodaboda - Baiskeli au pikipiki inayotumiwa kwa uchukuzi wa abiria

Mwananchi - Kwa maana ya mtu wa kawaida au raia wa kawaida

Daladala - (nchini Tanzania) mabasi madogo yanayotumiwa kwa uchukuzi wa abiria

Sambaza - Kugawa au kueneza kitu muhimu au cha thamani kwa watu wengine

Mwalimu - Neno linalotumiwa kabla ya kutaja jina la mtu anayeheshimika au anayeenziwa, ambaye anaweza kutoa ushauri au ujuzi kwa wengine. Mfano, Mwalimu Nyerere.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanzilishi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Maneno ya Kiswahili ambayo yamewahi kuingizwa kwenye kamusi za Kiingereza ni pamoja na Shamba na Safari.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii