Nigeria yaomboleza pamoja na Uingereza

Nigeria
Image caption Profesa ,Kaimu rais wa Nigeria Yemi Osinbajo

Kaimu rais wa Nigeria Yemi Osinbajo, amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelzwa dhidi ya watu wasio na hatia mjini Manchester, nchini Uingereza jana.

Kwa niaba ya raia wake na serikali ya Nigeria, Profesa Osinbajo ameonesha kusikitishwa kwake na tukio hilo na kutoa rambirambi na kuungana na serikali ya Uingereza na watu wake katika kipindi hiki cha maombolezo.

Akilielezea shambulizi hilo kuwa ni kitendo cha dharau na uhalifu wa kutisha ,Kaimu rais huyo Osinbajo amemhakikishia Waziri mkuu Theresa May kwamba sala, dua na fikra za wa Nigeria ziko pamoja na Waingereza wakati huu wakiomboleza tukio lililopoka uhai wa vijana wachanga .

Makamu raisi huyo ameeleza kuwa anaamini na ndiyo imani yake kuwa dunia iliyostaarabika milele mwanga wake utang'aa dhidi ya ulimwengu wa giza, na kwamba anaamini Uingereza na raia wake nan chi zingine kote ulimwenguni wataendelea kuonesha ustahamilivu na ujasiri katika harakati za kufutilia mbali makosa hayo ya jinai ya kigaidi.

Mwisho wa kauli yake amesema kwamba anamuomba mwenyezi Mungu awape faraja wafiwa na kuwaombea uponaji wa haraka majeruhi wote.