Sudan yakiuka vikwazo ilivyowekewa?

Rais wa Sudan Omar al Bashir Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Sudan Omar al Bashir

Ripoti mpya iliyotolewa inasema kwamba Sudan imeweza kukwepa vikwazo ilivyowekewa kimataifa na kizuizi cha kuingiza silaha.

Taasisi inayohusika na Utafiti wa masuala ya silaha na Migogoro yenye makao yake nchini Uingereza imesema inayo ushahidi kwamba Sudan imekuwa pia ikisambaza vifaa mbalimbali vya kijeshi katika makundi ya wapiganaji katika nchi mbalimbali za Afrika.

Taasisi hiyo ambayo inafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Uswisi imesema imepata utafiti wake huo ulioufanya katika silaha zilizokamatwa wazi kabisa jeshi la Sudan na waasi.

Awali, Sudan iliwahi kukanusha kuhusika na madai kama hayo.

Ripoti hizi mpya zimetolewa siku chache baada ya mapigano makali yaliyotokea katika jimbo la Darfur nchini humo.

Katika kuonekana kupingana na kauli hiyo awali Rais Omar al Bashir wa Sudan ameishutumu Misri kuunga mkono waasi ambao wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali yake katika jimbo hilo la Darfur.

Amesema wanajeshi wake wameyakamata magari hayo kutoka kwa waasi wakati wa mapigano makali yaliyotokea mwishoni mwa juma.

Hata hivyo, serikali ya Misri bado haijatoa kauli yoyote juu ya hilo.

Kwa upande wake Kiongozi wa waasi wa Darfur Min Minnawi amesema tuhuma kwamba Misri inawaunga mkono ni jambo la kupuuzwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii