Je unajua ni kwanini Flamingo husimama kwa guu moja?

Flamingo Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Ndege hao hawatumii nguvu nyingi wanaposimama kwa guu moja

Flamingo hutumia nguvu kidogo wanaposimama kwa guu moja, wanasayansi wamethibitisha.

Huenda ndivyo walivyozoeleka kuonekana wakisimama hivyo, lakini vipi na kwanini ndege hao husimama kwa guu moja bado ni kitendawili cha muda mrefu.

Sasa kundi kutoka Marekani limeonyesha kuwa flamingo hawatumii misuli yoyote wanaposimama kwa guu moja jambo linalomaanisha kuwa hawatumii nguvu nyingi sana.

Ni hali inayowaruhusu kusimama hivyo kwa guu moja kwa madaha huku wakisinzia.

Awali watafiti walishangaa iwapo kusimama hivyo kunasaidia kupunguza uchovu wa misuli wakati ndege hao walibadili kutoka kusimama kwa guu moja hadi jingine.

Makundi ya watafiti wengine yamegundua kuwa hali hii huwasaidia ndege hao kusawazisha ujoto wa mwilini.

Sasa profesa Young-Hui Chang, kutoka taasisi ya teknolojia ya Georgia (Georgia Tech) huko Atlanta, na Lena H Ting, wa chuo kikuu cha Emory, wamegundua siri ya mbinu hiyo.

Watafiti hao waliwafanyia uchunguzi kadhaa ndege walio hai na waliofariki. Na wamegundua kuwa Flamingo wanaweza kusimamishwa kwa gu moja pasi usaidizi wowote.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Unapomtizama ndege huyo usoni, anaposimama kwa guu moja, mguu uko chini ya mwili inayomaanisha kuwa mguu umejipinda kwa ndani. Inabidi usimame hivyo iliwa kuweza kuidhinisha mfumo wa kutua," Prof Chang ameiambia BBC.

Hatahivyo, ndege waliokufa hawawezi kusimama kwa miguu miwili, inayomaanisha jukumu kubwa la kutumika misuli katika kiwango hichi.

Watafiti hao pia waliwachunguza ndege walio hai, na kugundua kwamba wanaposimama kwa guu moja na kupumzika hawakusogea hata chembe. Jambo linalothibitisha u thabiti wa kusimama kwa aina hiyo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii