Trump 'kupigania amani'' baada ya kukutana na Papa

Donald Trump na Papa Francis wakiwa The Vatican Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump na Papa Francis wakiwa The Vatican

Rais Donald Trump ameapa kutumia wadhfa wake ili kukuza amani baada ya kile alichokitaja kuwa mkutano muhimu na Papa Francis mjini Vatican.

Katika chapisho la mtandao wake wa Twitter baada ya viongozi hao wawili kukutana, bwana Trump alisema kuwa ni heshima kubwa katika maisha yake kukutana na kiongozi huyo wa kanisa katoliki na kwamba amepata ari na azma ya kupigania amani duniani.

Wawili hao hapo awali walitofautiana vikali katika maswala kama vile Uhamiaji, hali ya hewa, na ujenzi wa ukuta wa Mexico.

Papa Francis amesema kuwa watu wanaojenga ukuta badala ya madaraja sio Wakristo.

Donald Trump alitaja matamshi hayo kama yasio na heshima.

Rais Trump sasa amewasili mjini Brussels kwa mazungumzo na Nato na maafisa wa EU.

Mada zinazohusiana