Yaya Toure na wakala wake wachangia wahanga wa shambulizi la Manchester

Toure ameleezea hisia zake juu ya tukio hilo kupitia kwa wakala wake Dimitri Seluk
Image caption Toure ameleezea hisia zake juu ya tukio hilo kupitia kwa wakala wake Dimitri Seluk

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure pamoja na wakala wake kwa pamoja wamechangia Paundi 100,000 kuwasaidia wahanga wa shambulizi la Manchester.

Takribani watu 22 walifariki na wengine 64 kujeruhiwa baada ya kijana Salman Abedi kujilipua katika uwanja huo siku ya Jumatatu.

Wakala wa Toure Dimitri Seluk ameiambia BBC kuwa wanataka kuwasaidia wahanga, familia za waliopoteza ndugu zao sambamba na wale waliopo hospitalini.

Anaongeza kuwa aliongea na Toure siku ya Jumanne na aliumizwa sana na tukio hilo, na hii ni kwasababu analipenda sana jiji la Manchester na watu wote.

Toure mchezaji tegemeo wa Manchester City, anatarajiwa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya hivi karibuni.