Roketi ya kwanza kabisa yarushwa kutoka New Zealand

Roketi ya kwanza kabisa yarushwa kutoka New Zealand Haki miliki ya picha Twitter/@RocketLabUSA
Image caption Roketi ya kwanza kabisa yarushwa kutoka New Zealand

Kampuni moja ya Marekani imerusha roketi kuenda anga za juu kutoka nchini New Zealand ambayo ni ya kwanza kutoka kituo cha kibinafsi.

Roketi hiyo iliondoka kutoka rasi ya Mahia katika kisiwa kilicho Kaskazini.

Jaribio hilo ndilo la kwanza kuwai kufanywa kutoka nchini New Zealand, linalotajwa kuwa hatua kubwa ya roketi kubeba satelaiti ndogo na mizigo mingine.

Haki miliki ya picha Rocket Lab
Image caption Roketi ya kwanza kabisa yarushwa kutoka New Zealand

Kampuni hiyo ina mipango ya kufanya shughuli za kibiashara za kurusha maroketi baadaye mwaka huu.

Jaribio hilo ambalo ni kati ya matatu yaliyopangwa, roketi haikubeba mzigo wowote lakini kampuni ya Rocket Lab inasema kuwa roketi hiyo itabeba kilo 150 kuenda kwa mzingo dunia.

Mwanzilishi wa kampuni ya Rocket Lab ambaye pia ni mkurungenzi mkuu ni raia wa New Zealand

Haki miliki ya picha Digital Globe
Image caption The launch site is located on North Island's Mahia peninsula