Ndege za Pakistan zatumiwa kusafirisha heroin hadi Uingereza

Heroin ilipatikana ndani ya dege ya Pakistan ambaye ingesafiri kuenda London Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Heroin ilipatikana ndani ya dege ya Pakistan ambaye ingesafiri kuenda London

Shirika la ndege la serikali nchini Pakistan, linasema kuwa linachukua hatua kuhakikisha kuwa ndege zake hazitumiwi kubeba madawa ya kelevya baada ya dawa ya heroin, kupatikana kwenye ndege zake mbili zinazofanya safari kuenda mjini London

Tarehe 15 mwezi huu wa Mei, maafisa wa mipaka wa Uingereza walikamata ndege iliyokuwa ikitokea mjini Islamabad ilipowasili uwanja wa Heathrow mjini London na kuikagua kwa saa kadhaa.

Shirika la kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza baadaye lilisema kuwa kiwango fulani cha heroin kilipatikana kimefichwa katika sehemu tofauti za ndege hiyo.

Kuna madai kuwa utawala nchini Uingereza ulichukua hatua hiyo kutokana na taarifa ulizopokea kutoka Pakistan.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Heroin ilipatikana ndani ya dege ya Pakistan ambaye ingesafiri kuenda London

Hakuna mtu aliyekamatwa lakini rubani wa ndege hiyo hakuruhusiwa kurudi Pakistan siku iliyofuata.

Kisa hicho kilisabisha aibu kwa shirika la ndege la Pakistan ambalo linapata nafuu baada ya ajali mbaya iliyowaua watu wengi mwezi Disemba,

Tarehe 22 mwezi Mei maafisa wa Pakistan katika uwanja wa ndege wa Islamabad, walikamata zaidi ya kilo 20 za dawa ya heroin ndani ya ndege nyingine iliyokuwa isafiri kuenda Heathrow.

Kwa sasa uchunguzi unafanyika kubaini ikiwa kuna ushirikiano wa kutumiwa ndega za shirika la ndege la Pakistan, kusafirisha madawa ya kulevya kuenda nchi za ng'ambo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mimea ya kuzalisha heroin inapatikana sehemu nyingi nchini Afghanistan

Mada zinazohusiana