Tizama ndani ya treni ya starehe ilioundwa India

Treni ya Tejas Express imeanza kazi na husafiri kati ya Mumbai na jimbo la kitalii Goa.

Abiria katika treni yaTejas Express kwenye safari ya kwanza

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Treni ya kwanza iliyoundwa India imeanza kufanya kazi. Tejas Express ina mabehewa yalio na viti vya starehena burudani ikiwemo filamu za Bollywood zinazoonyeshwa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Treni hiyo pia ina mtandao kupitia wi-fi, michezo ya kompyuta na pia mtu anaweza kusikiliza matangazo na muziki.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Treni ya Tejas Express thusafiri kwa saa nane na nusu kufika Goa kutoka Mumbai, hii ikiwa na kasi zaidi kidogo ikilinganishwana na treni nyingine.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Treni hiyo ina milango ya kufunguka wenyewe, otomatiki ni ya kwanza nchini India. Inaweza kwenda kwa mwendo kasi wa kilomita 200 kwa saa, lakini kuna udhibiti wa kasi wa treni nchini.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Inatarajiwa kuhudumu mara tano kwa wiki, kando na wakati wa msimu wa upepo mkali ambako itakuwa ikihudumu mara tatu kwa wiki.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kuna mashine za chakula na vinywaji kama chai na kahawa ndani ya treni.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

"Ni kama huduma ya ndege," abiria mmoja ameliamba shirika la habari AFP. "Nadhani hii treni ni fikra nzuri."

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Tiketi za kawaida huuzwa $18; huku za kiwango cha juu ni rupi 2,590

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Iwapo treni hiyo itapata umaarufu maafisa wanapanga kupanua huduma wakianza na jimbo jirani la Gujarat , ka mujibu wa taarifa.