Udhaifu wabainika kwenye vifaa vya kupima ubora wa afya

Je, vifaa hivi vinatoa vipimo halisi? Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je, vifaa hivi vinatoa vipimo halisi?

Utafiti umebaini kwamba vifaa vingi vya kupima ubora wa afya vinatoa takwimu za kupotosha kuhusu kiwango cha kalori kinachochomwa baada ya mazoezi.

Haya ni kulingana na uchunguzi wa vifaa hivyo katika chuo kikuu cha Stanford nchini Marekani.

Hata hivyo imebainika kwamba vifaa hivyo vina uwezo wa kupima mpigo wa roho kwa ufasaha.

Watafiti hao wanapendekeza kwamba wanaoutumia vifaa hivyo wawe waangalifu hususan wanapotumia vifaa hivyo kuchagua wanachokula.

Utafiti huo unapendekeza wanaotengeneza vifaa hivyo kutoa maelezo kamili ya jinsi wanavyotoa vipimo hivyo.

Vifaa vilivyofanyiwa utafiti ni Apple Watch, Fitbit Surge, Basis Peak, Microsoft Band, PulseOn na MIP Alpha 2.

Vifaa hivyo vilipatikana kuwa na makosa ya zaidi ya 20% katika kupima viwango vya nguvu ya mwili inayotumika katika mazoezi.

Daktari Euan Ashley wa chuo hicho cha Marekani anasema watumizi wa vifaa hivyo wanafaa kujuzwa manufaa na upungufu wa vifaa hivyo vinavyovaliwa mikononi.