Mwanamke Mhindi aliyelazimishwa kuolewa na Mpakistani arejea India

Uzma aliwasili India Alhamisi baada ya kuishi Pakistan mwezi mmoja Haki miliki ya picha RAVINDER SINGH ROBIN
Image caption Uzma aliwasili India Alhamisi baada ya kuishi Pakistan mwezi mmoja

Mwanamke huyo kutoka India anadai kwamba mwanamume huyo Mpakistani alitishia kumuua kwa kutumia bunduki iwapo angekataa kuwa mkewe.

Mwanamke huyo amerejea India siku moja baada ya uamuzi wa mahakama moja mjini Islamabad.

Mwanamke huyo, Uzma, alizindikishwa na maafisa wa ubalozi wa India nchini Pakistan.

Anasema mumewe,Tahir Ali, alimtesa

Tahir alikanusha madai hayo na kudai kwamba ni uongo mtupu.

Tukio hilo linajiri wakati mzozo kati ya mataifa hayo unazidi kutokota.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe wa waziri wa mambo yaa kigeni wa India

Waziri wa maswala ya kigeni nchini India, Sushma Swaraj, alimkaribisha mwanamke huyo kwa ujumbe kwenye mtandao wa Twitter.

"Uzma - Karibu nyumbani binti wa India. Pole kwa masaibu yaliyokukumba"

Mzozo kati ya India na Pakistan unachochewa na vurugu zinazoshuhudiwa katika eneo la Kashmir linalozozaniwa na mataifa hayo.

Mada zinazohusiana