Monaco yamsajili mchezaji kinda wa mwaka nchini Ubelgiji Youri Tielemans

Youri aliisaidia Anderlecht kufikia hatua ya robo fainali michuano ya Europa
Image caption Youri aliisaidia Anderlecht kufikia hatua ya robo fainali michuano ya Europa

Monaco imemsajili mchezaji bora kinda wa mwaka nchini Ubelgiji, Youri Tielemans kutoka klabu ya Anderlecht kwa pauni milioni 21.63.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, aliridhia mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa nchini Ufaransa.

Alifunga magoli 13 kwenye michuano magoli 13 msimu uliopita na kuifanya Anderlecht kutwaa ubingwa.

Monaco ni klabu yenye malengo, inayotambulika kwenye michuano ya Ulaya na mara nyingi hutumia wachezaji chipukizi.