Steve Cook atia saini mkataba mpya na Bournemouth

Cook alifungia magoli mawili Bournemouth msimu wa mwaka 2016-2017 Haki miliki ya picha PA
Image caption Cook alifungia magoli mawili Bournemouth msimu wa mwaka 2016-2017

Mlinzi wa klabu ya Bournemouth Steve Cook ametia saini mkataba mpya wa miaka minne na timu hiyo.

Mlinzi huyo wa kati amecheza michezo yote ya msimu huu wa ligi.

''umekuwa ni mpango wangu kuendelea kubaki hapa, ili niweze kupatiwa nafasi ya kufanya hivyo ni jambo la kufurahisha'' alisema Cook.

Cook amecheza klabuni hapo mara 231 tangu aingie Bournemouth akitokea Brighton katika msimu wa joto mwaka 2011.

''Mimi na Bournemouth tumekuwa tukipatana ''Cook alisema ''tangu Kocha alipokuja mambo yamekuwa yakisonga mbele tu hali ambayo imekwenda sambamba na matarajio yangu''.