Manchester United yawakumbuka waathirika wa shambulizi

Wachezaji wa Manchester United wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mchezo wa siku ya Jumatano
Image caption Wachezaji wa Manchester United wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mchezo wa siku ya Jumatano

Manchester United imetumia ushindi iliyoupata kwenye ligi ya Europa kuwakumbuka waathirika washambulio la siku ya Jumatatu mjini Manchester, kwa kutoa salamu za rambirambi.

Ushindi wa United wa mabao 2-0 dhidi ya Ajax mjini Stockholm umekuja siku mbili baada ya watu 22 kuuawa kwa bomu la kujitoa muhanga kwenye jumba moja la maonyesho mjini Manchester.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema ''pangelikuwa na uwezo wa kubadilisha maisha ya waliokufa, tungelifanya hivyo mara moja''.

Klabu ya Manchester iliweka picha ya bango kwenye akaunti yake ya Tweeter iliyoandikwa Machester -mji ulio na umoja''

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema ''kama tungeweza kubadili maisha tungefanya hivyo haraka sana''

Mshambuliaji mzaliwa wa jiji la Manchester Marcus Rashford amesema ushindi wao ni kwa ajili ya mji wa Manchester huku mchezaji ghali zaidi duniani, Paul Pogba akisema ''tulicheza kwa ajili ya watu waliopoteza maisha''.

Nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney amewataka watu kuchangia kusaidia familia za walioathirika.