Australia: Uwanja wa gwiji Margaret Court Arena hautabadilishwa jina

Margaret Court alishinda mataji 11 ya Australian Open
Image caption Margaret Court alishinda mataji 11 ya Australian Open

Uwanja wa michezo wa Australian Open uliokuwa ukiitwa Margaret Court Arena hautaitwa jina jingine licha ya Margaret ambaye ni mshindi mara 24 wa Grand Slam kupinga ndoa za jinsia moja.

Margaret raia wa Australia mwenye miaka 74 ambaye kwa sasa ni mchungaji, amesema ikiwezekana pia hatosafiri kwa ndege za Qantas ikiwa ni hatua ya kupinga shirika hilo kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja.

Chama cha Tenisi cha Australia kimesema hayo ni mawazo yake na hakuna wa kumuingilia.

Washindi wa Grand Slam Martina Navratilova na Billie Jean King ambao wote wanaunga mkono mapenzi ya jinsia moja wameikosoa vikali mahakama kwa kitendo cha kubadilisha jina la uwanja huo.

Uwanja huo awali uliitwa Show Court One ulipofunguliwa mwaka 1988 kabla ya mwaka 2003 kubadilishwa jina na kuitwa Margaret Court Arena ikiwa ni heshima ya gwiji huyo.

Uwanja wa Margaret Court Arena pia hutumikwa kwa ajili ya michezo mingine pamoja na matamasha mbali mbali.