Nchi 40 za Afrika kusheherekea Azimio la Kilimanjaro

arusha
Image caption Wakazi wa Arusha nchini Tanzania wakisheherekea azimio la kilimanjaro katika maadhimisho ya siku ya ukombozi wa Africa

Siku ya maadhimisho ya ukombozi wa Afrika,mwaka huu imesheherekewa kwa kuzinduliwa rasmi azimio la kilimanjaro ambalo ni mwamko wa waafrika katika kupigania haki, amani na heshima.

Afrika arising au mwamko wa Afrika ni harakati zinazo waunganisha waafrika kupitia mitandao ya kijamii,majukwaa,makongamano na matamasha ambayo yameandaliwa na makundi mbalimbali ya kijamii katika nchi mbalimbali za Afrika.

Haki miliki ya picha africa rising
Image caption Baadhi ya vijana,mjini Arusha nchini Tanzania, wakisheherekea siku ya ukombozi wa Afrika

Azimio la Kilimanjaro limeweza kuunganisha makundi mbalimbali ya jamii,wengi wao wakiwa vijana kutoka mataifa 40 ya Afrika huku mataifa yote yakiwa na dhana ya kuimarisha ukombozi halisi wa bara Afrika ili kuipata Afrika wanayoitaka.

Misingi ya harakati hizi ambazo zinawasilishwa kwa njia ya Amani ni kusisitiza haki za msingi kwa waafrika kutoka kwa viongozi wao na serikali zao .

Pamoja na kuwa harakati za Afrika zilikuwepo wakati wa kupigania uhuru lakini sasa mwamko wa Afrika ,unataka kulaani unyonyaji wa raslimali na mali asili ,ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.