Jeshi la Ufilipino lafanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS

Vikosi vya jeshi vikiwasaidia wakazi wa Maravi kuelekea sehemu salama
Image caption Vikosi vya jeshi vikiwasaidia wakazi wa Maravi kuelekea sehemu salama

Vikosi vya jeshi la Ufilipino vimeanza kutumia mashambulizi ya anga kukabiliana na vikosi vya IS vilivyojichimbia Mashariki mwa nchi hiyo.

Uvamizi huo ulikwenda kinyume na matarajio, jambo lililopelekea mamia ya wanajeshi kuweka kambi maalum katika mji wa Maravi, huku wakitumia mabomu katika harakati za kupambana na wanamgambo hao jambo lililopelekea vifo vya watu 20.

Wanajeshi wa Philipines wamesema kazi sio nyepesi huku mapigano yakiendelea.

Image caption Vikosi hivyo vimesema vinakabiliana na wapiganaji kati ya 30 mpaka 40

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema sheria za kijeshi ni lazima kuanzishwa katika eneo hilo na maeneo ya jirani ili kuondoa kabisa ongezeko la wapiganaji wa Islamic State.

Mmoja wa wamiliki wa kituo cha kuuza mafuta kilichopo eneo hilo aitwae Anwar amesema mapigano hayo yanahatarisha maisha yake.

Rais wa Philipines Rodrigo Duterte tiyari ametangaza hali ya hatari katika eneo hilo na sambamba na kuongeza vikosi vya kijeshi kukabiliana na wapiganaji hao, huku pia ikishuhudiwa mamia kwa mamia ya watu wakiyahama makazi yao.

Mada zinazohusiana