Wanawake waliofanywa watumwa wa ngono wa al-Shabab

Wanawake waliofanywa watumwa wa ngono wa al-Shabab

BBC imewagundua na kuzungumza kwa mara ya kwanza na wanawake Wakenya waliotoroka utumwa wa kingono kutoka kambi za wapiganaji wa Al-Shabab Somalia.

Katika uchunguzi wa kipekee mwandishi Anne Soy amezungumza na kikundi cha wanawake ambao waliathirika na biashara haramu ya binadamu na kusafirishwa hadi Somalia na kunajisiwa.

Tumebadilisha majina yao kwa sababu za usalama wao.