FBI wamchunguza mkwe wa Trump, Kushner

Rais Trump na mkwe wake Jared Kushner Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Trump na mkwe wake Jared Kushner

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa Mkwe wa Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye pia ni mshauri wake mwandamizi Jared Kushner anachunguzwa na Shirika la upelelezi nchini humo FBI, juu ya tuhuma za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa nchi hiyo mwaka uliopita.

Habari zinasema wachunguzi wanaamini kuwa Kushner anaweza kuwa na taarifa za uhakika kuhusiana na uchunguzi wao, lakini hatua hiyo sio lazima kumfanya kuwa yeye ni mshukiwa wa uhalifu.

Kushner anafahamika pia kwamba mwaka uliopita alikutana na balozi wa Urusi Sergei Kslyak pamoja na Mwenyekiti wa bodi, benki ya Urusi Sergei Gorkov.

Hata hivyo mwanasheria wake anasema mteja wake tayari alijitolea kuzungumza na bunge la Congress juu ya nini anachojua kuhusiana na mikutano hiyo yote ya viongozi hao.