Polisi Uingereza yamkamata mtu wa kumi

Mwanajeshi wa kikosi cha kutegua mabomu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanajeshi wa kikosi cha kutegua mabomu

Polisi wamemkamata mtu mmoja mjini Manchester akihusishwa na shambulizi lilitokea jumatatu mjini humo, shambulio lililogharimu maisha ya watu 22.

Polisi mjini humo wamesema ni mmoja kati ya watu wanane ambao wako chini ya ulinzi kwa uchunguzi.

Polisi wanaamini kuwa mtu aliyejitoa muhanga Salman Abedi, 22 ametokea katika familia yenye asili ya Libya ,na alikuwa sehemu ya mtandao uliohusika na shambulizi hilo.

Kwa jumla watu 10 wameshikiliwa Uingereza lakini wawili waliachiwa baadae.

Uingereza hali bado si shwari hii inamaanisha shambulio jingine linaweza kutokea.