Wakristo 23 wa madhehebu ya Coptic wauwawa Misri

Mauwaji Misri
Image caption Mauwaji Misri

Watu wenye silaha nchini Misri, wameshambulia basi moja lililokuwa limewabeba wakristo wa dhehebu la Coptic na kuwauwa watu kadhaa.

Gavana wa jimbo hilo, anasema kuwa watu 23 walimiminiwa risasi na kuuwawa, huku wengine wapatao 25 wakijeruhiwa, katika shambulio hilo lililofanyika kusini mwa Misri.

Wakristo wa dhehebu la Coptic nchini Misri, wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara, hasa katika miezi ya hivi karibuni, ambapo tawi la kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Misri, wamekiri kutekeleza mashambulio hayo.

Mnamo Aprili mwaka huu, watu 40 waliuwawa, baada ya makanisa ya Coptic yalipolipuliwa mabomu.

Mada zinazohusiana