Afrika wiki hii kwa picha: 19 - 25 Mei 2017

Baadhi ya picha bora kutoka barani Afrika na zile za Waafrika wakiwa sehemu mbali mbali duniani.

Jamaa za wasichana 82 wa Chibok walioachiliwa mwezi Mei wanasalimiana huku wakingojea kukutana nao eneo la Abuja, Nigeria Mei 20, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakati wa kusherehekea kwa jamaa za wasichana 82 wa Chibok walioachiliwa mwezi Mei, huku wakingojea kukutana nao.
Baba anakutana na mwanawe, mmoja wa wasichana wa Chibok walioachiliwa. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ulikuwa mkutano wenye hisia nyingi kwa familia ambao walisafiri kutoka jimbo la kaskazini-mashariki la Borno hadi mji mkuu, Abuja...
Jamaa wanakutana na wasichana wao walioachiliwa. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wale walioachiliwa ni miongoni mwa wasichana 276 wa shule waliotekwa nyara na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram mwaka wa 2014 kutoka shule ya serikali katika mji wa Chibok.
Watu wanashikilia mabango yaliyo na picha ya mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus kutoka Ethiopia wakati wa mkutano wa hadhara, mbele ya ofisi za Umoja wa Mataifa. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku ya Jumanne, raia wa Ethiopia wanakusanyika nje ya makao makuu ya Shirika la Afya Duniani mjini Geneva, Uswisi, ili kumuunga mkono Tedros Adhanom Ghebreyesus, kiongozi mpya wa WHO, na mwafrika wa kwanza kuongoza shirika hilo.
Wafuasi wa Meya wa Dakar Khalifa Sall wabeba mabango katika maandamano ya kuitisha kuachiliwa kwake. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafuasi wa Meya wa Dakar Khalifa Sall, ambaye anazuiliwa kwa mashtaka ya udanganyifu na fedha chafu, wafanya maandamano katika mji mkuu wa Senegal wakkitisha kuachiliwa kwake.
Muuzaji nchini Misri anafuta vumbi kutoka kwenye taa ya jadi ya Ramadhani au "fanous" katika duka lake Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Siku ya Jumatano, muuzaji nchini Misri anafuta vumbi kutoka kwenye taa ya jadi ya Ramadhani au "fanous" katika duka lake kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mjini Cairo...
Wanawake wa Misri wabeba Fanous kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mjini Cairo... Mei 24, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Fanous ni ishara ya matumaini na hutumiwa kama pambo wakati wa Ramadhan.
Mwanamke anunua pakiti ya unga wa mahindi iliyotolewa ruzuku na serikali katika maduka makubwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, siku ya Jumatano. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamke anunua pakiti ya unga wa mahindi iliyotolewa ruzuku na serikali katika maduka makubwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, siku ya Jumatano.
Mama ananunua matunda kutoka kwa muuzaji Harare, Zimbabwe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakati huo huo, katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, mama huyu ananunua matunda kutoka kwa muuzaji mitaani.
Roboti inatumiwa katika mashindano ya kitaifa k tarehe 20 Mei, 2017 katika uwanja wa Marius Ndaye katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Fainali za mashindano ya kitaifa ya roboti iliyofanyika mjini Dakar Jumamosi ...
Roboti inatumiwa katika mashindano ya kitaifa k tarehe 20 Mei, 2017 katika uwanja wa Marius Ndaye katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hafla hii imeandaliwa na serikali ya Senegal ili kuwapa vijana motisha ya kusomea sayansi...
Roboti inatumiwa katika mashindano ya kitaifa k tarehe 20 Mei, 2017 katika uwanja wa Marius Ndaye katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanafunzi wengi walifanya maonyesho katika mashindano hayo katika uwanja wa Marius Ndaye ambao hutumiwa kwa mchezo wa kikapu.
Roboti inatumiwa katika mashindano ya kitaifa k tarehe 20 Mei, 2017 katika uwanja wa Marius Ndaye katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Roboti yaonesha jinsi inaweza kutenda mambo.
Wakazi wa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini ulioathiriwa na ukame wanachota maji safi kwenye mkondo eneo la Table Mountain Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakazi wa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini ulioathiriwa na ukame wanachota maji safi kwenye mkondo eneo la Table Mountain

Wakazi wa ukame hit Cape Town nchini Afrika Kusini umati karibu na chanzo cha maji safi kutoka kwenye mkondo mbali Table Mountain kukusanya maji salama ya kunywa wakati wa usiku.

Siku ya Ijumaa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Mali Rais Ibrahim Boubacar Keita wakikagua walinzi wa heshima wakati wa ziara yake Gao, kaskazini mwa Mali. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku ya Ijumaa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Mali Rais Ibrahim Boubacar Keita wakikagua walinzi wa heshima wakati wa ziara yake Gao, kaskazini mwa Mali.

icha ni kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images na Reuters