Bomba la kupitisha pombe kujengwa Ujerumani

Pombe itakuwepo kwa wingi katika tamasha hilo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pombe itakuwepo kwa wingi katika tamasha hilo

Waandalizi wa Tamasha maarufu la muziki wa rock nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja zaidi ya elfu 75 kwamba, katu! hawatokumbwa na kiu ya pombe.

Wanajenga bomba kubwa la kusafirisha pombe katika eneo la tamasha hilo.

Waandalizi wa tamsha hilo maarufu kwa jina, Wacken Open Air festival, wanasema bomba hilo litakuwa na uwezo wa kufikisha glasi sita za pombe kwa kila sekunde.

Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na upana wa inchi 14.

Haki miliki ya picha WOA WEBSITE
Image caption Bomba hili litazuia uharibifu unaotokana na mgari ya kusafirisha pombe kila siku

Watu elfu 75 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwaka, na inakadiriwa kwamba kila mmoja huwa anabugia lita tano za pombe katika kipindi cha siku tatu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zaidi ya watu 75,000 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwaka