Dwayne 'The Rock' Johnson kuwania urais Marekani mwaka 2020?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwigizaji na mwanamiereka Dwayne 'The Rock' Johnson

Dwayne 'The Rock' Johnson kuwania urais mwaka 2020?

Dwayne 'The Rock' Johnson alitangaza kuwa atawania urais wa Marekani mwaka 2020 wakati akitumbuiza mashabiki wake katika kipindi maarufu cha Saturday Night Live.

Mwigizaji maarufu Tom Hanks alikubali kuwa naibu rais.

Baadaye, mwigizaji huyo anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ulimwenguni alisema tangazo hilo lilikuwa la utani.

Hata hivyo alisisitiza kwamba "Marekani inahitaji viongozi walio na uwezo wa kuongoza, wanaojali maslahi ya taifa hili na raia wake"

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Korongo waliokufa wana uwezo wa kusimama kwa mguu mmoja!

Korongo waliokufa wana uwezo wa kusimama kwa mguu mmoja!

Wanasayansi wamegundua kwamba korongo huwa wanahifadhi nguvu nyingi za mwili wanaposimama kwa mguu mmoja.

Ndege hao ni maarufu kwa mtindo wao wa kusimama kwa mguu mmoja, japo kwa muda mrefu sababu ya mtindo huo imekuwa kizungumkuti kwa muda mrefu.

Wanasayansi wa Marekani wanasema kwamba ndege hao huwa hawatumii nguvu nyingi za misuli wanaposimama na mguu mmoja ikilinganishwa na wanaposimama kwa miguu miwili.

Haki miliki ya picha DUBAI MEDIA OFFICE
Image caption Taarifa inayokusunywa na roboti hiyo itasambazwa kwa maafisa wa usafiri na trafiki.

Roboti inayohudumu kama polisi yazinduliwa Dubai

Polisi nchini Dubai wamezindua afisa roboti ya kwanza itakayo piga doria katika majumba ya kibiashara na maeneo ya kivutio kwa watalii.

Watu wataweza kuripoti uhalifu, kulipa faini na kupata taarifa kwa kugusa kompyuta iliopo kifuani mwa roboti hiyo.

Taarifa inayokusunywa na roboti hiyo itasambazwa kwa maafisa wa usafiri na trafiki.

Image caption Ubongo wa binadamu una hisia ya sita yenye uwezo wa 'kubashiri' matukio ya baadaye.

Ubongo wa binadamu una hisia ya sita yenye uwezo wa 'kubashiri' matukio ya baadaye.

Kando na kusaidia kutambua unachoona kupitia kwa macho , upande maalum wa ubongo unaosaidia kuona una uwezo wa kubashiri matukio ya baadaye.

Wataalm wa ubongo kutoka chuo kikuu cha Radboud University waligundua hisia hiyo ya sita baada ya utafiti wa kina.

Haya ni kulingana na mtandao wa Huffington post.

Unajua kuna mananasi yenye rangi ya waridi?

Wengi wanafahamu manansi yenye rangi ya dhahabu.

Hata hivyo, kulingana na mtandao wa habari wa Evening standard, picha za mananasi yenye rangi ya waridi zimeibuka kwenye Instagram na kusababisha msisimko mkubwa.

Sio ngozi yake pekee iliyo na rangi hiyo, mbali pia unapokata mananasi hayo, unakumbana na rangi ya waridi.