Viongozi wa G7 waangazia bara la Afrika

Viongozi wa G7 wanaliangazia bara la Afrika hususan swala la wahamiaji wanaoingia Afrika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wa G7 wanaliangazia bara la Afrika hususan swala la wahamiaji wanaoingia Afrika

Viongozi kadha wa nchi za Afrika wanahudhuria siku ya pili ya mazungumzo katika mkutano huo wa G7, ili kujadili tatizo la wahamiaji.

Itali iliamua kuandaa mkutano huo huko Sicily, ili kuvutia macho ya ulimwengu juu ya shida za Waafrika wanaohatarisha maisha yao, kuvuka Mediterranean ili kuingia Ulaya.

Tayari mwaka huu, wahamiaji elfu hamsini wameingia Italia, huku 1500 wamezama safarini.

Kwa hivyo viongozi wa G7 wamezungumza na wenzao kutoka Tunisia, Kenya, Ethiopia, Niger na Nigeria, kutafuta njia za kuhimiza maendeleo Afrika, ikitarajiwa kuwa itawafanya wahamiaji wabaki makwao.

Lakini juhudi za Itali, za kutaka G7 kukubali kupokea wahamiaji zaidi, inaelekea zitapingwa na hasa Marekani.