Usafiri wa ndege warejea kawaida Uingereza

Abiria nje wa unanja wa Gatwick Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Abiria nje wa unanja wa Gatwick

Huduma za usafiri katika viwanja vya ndege vya uingereza vya Gatwick naHeathrow zimerejea kama kawaida baada ya hitilafu za mitambo kulemaza huduma hizo hapo jana na kuathiri maelfu ya abiria kote ulimwenguni.

Hitilafu hiyo ambayo haikutarajiwa imesababisha hasara kubwa kutokana na gharama kubwa ya fidia kwa wasafiri, na matatizo ya kimikakati ya ndege, mizigo na watu..

Kampuni ya usafiri wa ndege ya British Airways imewataka watu kudhibitisha iwapo wamepewa nafasi ya kiti ndani ya ndege kabla ya kuelekea uwanja wa ndege.

British Airways inasema kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa hitilafu hiyo ilisababioshwa na udukuzi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Abiria waliachwa wamekwama nje wa uwanja wa Heathrow

Mkurugenzi mkuu Alex Cruz alisema inaaminika kuwa sababu kuu ya tatizo hilo ni suala la umeme.

Mashirika mengine yanayotoa huduma kupitia viwanja hivyo viwili hayakuathirika.

Tatizo liliathiri maeneo ya kuingia abiria, huduma za wateja na simu.