Picha za aliyefanya shambulizi Manchester zatolewa

Picha za Salman Abedi Haki miliki ya picha Greater Manchester Police
Image caption Picha za Salman Abedi

Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.

Maeneo 14 yanasakwa na wanaume 11 wamekamtwa kwa kushukiwa kuhusika katika ugaidi.

Abedi alitambuliwa saa mbili baada ya shambulizi la siku ya Jumatatu.

Waziri mkiu Theresa May anasema kuwa kiwango cha tisho lililopo kimepunguzwa na wanajehsi waliotumwa kuwasaidia polisi wataondolewa kuanzia siku ya Jumatatu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ulinzi mkali uliwekwa Wembley

Mamia ya polisi waliojihami wanaendelea kulinda mamia ya tamasha kote nchini Uingereza.

Mamia ya polisi walitumwa wakati mashabiki 50,000 walihudhuriw tamasha la Courteeners kwenye uwanja wa kriketi wa Old Trafford, ambalo ni tamasha kubwa kufanyika mjini humo tangu shambulizi kutokea.

Ulinzi zaidi umewekwa leo wakati wa mbio za Great Manchester Run ambapo maelfu ya wanariadha wanatarajiwa kushirikia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Jumamosi polisi walivamia eneo la Moss Side huko Manchester