Raia wakambwa na hatari kubwa Mosul, Iraq

Wanajeshi wanasema kuwa wamepiga hatua kwa saa chache wanapojaribu kuwatimua wanamgambo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wanasema kuwa wamepiga hatua kwa saa chache wanapojaribu kuwatimua wanamgambo

Huku vita kati ya serikali ya Iraq na wapiganaji wa Islamic state vikiendelea kushika kasi mjini Mosul, raia waliokwama katika mji huo watakabiliwa na majanga makubwa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kulingana na Mratibu wa misaada ya kibinadam wa umoja huo, Lise Grande, raia wa Mosul wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, maji, dawa na umeme.

Raia wanaojaribu kutoroka wanauwawa na Islamic state.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rai wakwama Mosul huku mapigano yakiendelea

Kumeibuka ripoti kwamba walenga shabaha wa Islamic state wamekuwa wakiwauwa watoto kimakusudi.

Wanajeshi wanasema kuwa wamepiga hatua kwa saa chache wanapojaribu kuwatimua wanamgambo hao kutoka ngome zao za mwisho katika mji wa zamani wa Mosul.

Maelf ya raia wameukimbia mji huo wa kaskazini tangu jitihada za kuukomboa zianze mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano ya Mosul yamesababisha kuhama zaidi ya watu 500,000