Trump na Macron walisamiana vipi Brussels?

Trump na Macron walisamiana vipi Brussels? Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump na Macron walisamiana vipi Brussels?

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amekiri kuwa, mkono wa nguvu aliompa Rais Donald Trump katika mkutano wa NATO mjini Brussels siku ya Alhamisi, ulikusudiwa kuwa hivyo.

Mkono huo aliompa Rais Trump umezungumzwa sana.

Bwana Macron aliliambia gazeti moja la Ufaransa, alitaka kuonesha kuwa Ufaransa haitoridhia vitu vidogo hata kama havina maana.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump na Macron walisamiana vipi Brussels?

Wadadaisi wanasema Rais Trump anapompa mtu mkono, ana tabia ya kumvuta yule mtu kwake, kuonesha nani anamshinda mwenzake kwa nguvu na hadhi.

Viongozi hao walikutana mjini Brussels kabla ya kufanyika mkutano wa NATO

Wakatai wawili hao wakisalimiana kwa sekunde kadha bwana Macron na Trump waliangaliana macho kwa macho kwa muda hadi pale Trump alijaribu kuangalia kando