Merkel azitaka nchi za Ulaya kujitegemea

Angela Merkel amesema mkutano wa G7 wa mwaka huu ulikua na changamoto zaidi
Image caption Angela Merkel amesema mkutano wa G7 wa mwaka huu ulikua na changamoto zaidi

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezionya nchi nyingine za umoja wa Ulaya kwamba kwamba muda umefika wa kupunguza utegemezi.

Akiongea baada ya mkutano wa nchi saba zilizoendelea kiviwanda zaidi duniani (G7), mkutano alioutaja kama wenye changamoto zaidi, amesema nchi za Ulaya zinapaswa kufanya mambo yao wenyewe huku zikibaki kuwa marafiki wa karibu kwa Uingereza na Marekani.

Katika mkutano huo uliofanyika nchini Italia, Rais Trump alikataa kuidhinisha mkataba wa mkutano wa Paris juu ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.