Brazil: Michel Temer amuondoa kazini waziri wa sheria

Temer amesema hawezi kuondoka madarakani kwa kashfa hiyo
Image caption Temer amesema hawezi kuondoka madarakani kwa kashfa hiyo

Rais wa Brazil Michel Temer amemuondoa kazini waziri wa sheria ikiwa ni hatua yake kukabiliana na kashfa ya rushwa inayomuandama.

Nafasi ya Osmar Serraglio inachukuliwa na Torquato Jardim.

Hakuna sababu iliyotolewa kwa mabadiliko hayo.

Rais Temer anachunguzwa na mahakama kuu ambayo imetoa ushahidi kuwa alipokea mamilioni ya dola kama rushwa.

Temer ameapa kujibu tuhuma hizo huku ikishuhudiwa vyama kadhaa vinayounda muungano wa serikali yake vikijiondoa huku maandamano makubwa yakifanyika nchi nzima.