Mamia ya waandamanaji wafunga barabara za mitaa Rabat, Morocco

Vyombo vya habari nchini Morocco vinasema kuwa ni nadra sana kwa maandamano kutokea nchini humo
Image caption Vyombo vya habari nchini Morocco vinasema kuwa ni nadra sana kwa maandamano kutokea nchini humo

Mamia ya waandamanaji nchini Morocco wamefunga mitaa maarufu katika mji mkuu wa nchi hiyo Rabat, huku maandamano mengine yakiendelea Kaskazini mwa nchi hiyo kwa miezi saba sasa.

Kumekuwa na hali ya wasi wasi tangu siku ya Ijumaa pale vurugu zilipozuka nje ya mji wa al-Hoceima baada ya polisi kujaribu kumshikilia mwanaharakati maarufu Nasser Zefzafi.

Inadaiwa kuwa mwanahakati huyo alivuruga ibada iliyokuwa ikiendelea katika moja ya msikiti.

Image caption Nasser Zefzafi ni kiongozi wa maandamano hayo akitaka kuboreshwa kwa hali ya maisha katika mji wa Rif

Vyombo vya habari kutoka nchini humo vinasema kuwa ni nadra vurugu kutokea nchini Morocco.

Hata hivyo hali imekuwa mbaya tangu mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na kisa cha mfanyabiashara maarufu wa samaki al-Hoceima aliyeuawa wakati akiwazuia maofisa wa serikali wasiharibu ghala la samaki wake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii