Mashujaa waliomtetea kijana wa kiislamu kutunukiwa Portland

Portland
Image caption Talesin Myddin aliuwawa katika shambulio,Portland

Zaidi ya dola laki sita za Kimarekani zimechangishwa kwa ajili ya kuzisaidia familia za watu watatu waliokamatwa wakati wakimsaidia kijana mmoja wa kiislamu pamoja na rafiki yake katika gari moshi.

Talesin Myddin,Namkai Meche na Ricky John Best waliuwawa ,huku Micah David-Cole Fletcher walijeruiwa vibaya huko Portand ,Oregon siku ya Ijumaa.

Hao wote walijumuishwa baada ya mabishano makali juu ya kupinga uvaaji wa hijabu kwa vijana wadogo. Watuhumiwa Jeremy Joseph Christian walikamatwa baadae.

Hata hivyo, mtu mwenye umri wa miaka 35 anatarajiwa kufika mahakamani siku ya Jumanne, akituhumiwa kwa madai ya mauaji, jaribio la kuua,kushurutisha na kuwa jambazi anayemiliki silaha kali.

Image caption Jeremy Joseph Christian,mtuhumiwa wa shambulizi

Shririka la kijasusi la Marekani FBI, limesema bado halina uhakika kama Christian ambaye alitamka kwamba ''waislamu wote wauwawe'' wakati wa shambulio hilo ataweza kuhukumiwa kwa kosa linalosababishwa na chuki.

Mpaka sasa kijana aliyejeruhiwa, Fletcher anaendelea vizuri na matibabu na hata ameweza kutuma picha yake mtandaoni akiwa amelala hospitalini na kuandika shairi linalosema, ''nimepambana na jicho la chuki na bado naishi.''

Wakati huo huo, watu watatu waliosaidia katika uokozi wa vijana hao wamepokelewa na jamii inayowazunguka kwa shangwe na kuonekana kuwa ni mashujaa.