Idara ya Usalama nchini Uingereza MI-5 kujichunguza

mi
Image caption Idara ya usalama,MI-5

Idara ya usalama nchini Uingereza MI5 wameamua kuchunguza njia ambazo zinatumika kupokea au kutoa taarifa kwa umma mara baada ya shambulio la mauaji lililotokea jumatatu iliyopita na kusababisha vifo vya watu ishirini na wawili.

Uchunguzi huo utaangazia namna ambavyo MI5 ilishindwa kupata taarifa za vitisho zilizotolewa na Salman Abedi licha ya kuwa tahadhari tatu za awali juu ya uvamizi huo wa hatari zilipatikana.

Kati ya watu kumi na sita waliokamatwa kuhusika na tukio la shambulizi wiki iliyopita,watu kumi na nne bado wanaendelea kushikiliwa na polisi.

Na huku Uchunguzi bado unaendelea katika eneo la Manchester,kaskazini mwa Uingereza