Mwanamke aliyefanywa mtumwa na al-Shabab asimulia

Mwanamke aliyefanywa mtumwa na al-Shabab asimulia

Faith alikuwa na umri wa miaka 16 alipotekwa na wanachama wa kundi la al-Shabab na kufanywa mtumwa wa ngono.

Ametoroka baada ya kuwa mtumwa wa al-Shabab kwa miaka mitatu

“Tulibakwa ndani ya chumba kimoja. Baada ya hapo sijui walitupea nini. Nilipopata fahamu tena nilijipata msituni,” anasema.

Faith alichukuliwa kutoka Kenya hadi katika msitu wa Boni ulio mpakani mwa Kenya na Somalia ambapo alitendewa ukatili huo.