Jeshi la Ufilipino laahidi kushinda vita dhidi ya waasi

Jeshi
Image caption Jeshi la Ufilipino

Jeshi la Ufilipino limesema kwamba litashinda mapigano kati yao na waasi wa kiislamu waliokuwa wameshikilia eneo la kusini mwa mji wa Marawi wiki moja iliyopita.

Kulingana na taarifa za jeshi hilo, wapiganaji wa Maute kwa sasa wanashikilia eneo dogo katika mji huo.

Ndege za kivita na mabomu yameelekezwa kwa waasi hao.

Mamia ya watu bado wanadhaniwa kushikiliwa katika mji wa Marawi na baadhi yao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu wakiomba msaada kwa mamlaka husika.

Takribani watu 19 wamefariki. Mapigano yalianza pindi jeshi lilipomshikilia kiongozi wa waasi hao.