Al-Shabab waua mzinifu kwa mawe

Al-shabab Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Al-shabab

Wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia wamempiga mtu mmoja na kumuuwa mara tu baada ya kuhukumiwa na mahakama ya kiislamu kwa kosa la uzinzi.

Dayow Mohamed Hassan mwenye umri wa miaka 44 aliuwawa kwa kunyongwa na kushambuliwa kwa mawe na wapiganaji wa Alshabab.

Hassan alishtakiwa kwa kosa la kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanamke ambaye sio mke wake na kumpa mimba huku akiwa na wake wawili wa ndoa.

Wapiganaji wa kiislamu wa Alshabab, wamekuwa wakitoa adhabu za aina hiyo mara kwa mara ili kukomesha uzinifu nchini Somalia.

Mwaka 2014, kijana mdogo alipigwa mawe mpaka kufa baada ya kukutwa na kosa la kubaka.

Miaka 4 baadae, msichana mdogo aliuwawa mara baada ya kushitakiwa kwa kosa la kuwa mzinzi.