Hofu ya kimbunga yahamisha maelfu ya watu pwani ya Bangladesh

Maeneo haya hukumbwa na kimbunga mara kwa mara
Image caption Maeneo haya hukumbwa na kimbunga mara kwa mara

Maelfu ya wakazi wa pwani ya Bangladesh wanahamishwa baada ya kimbunga chenye nguvu kuonekana kuelekea katika maeneo hayo.

Kinatarajiwa kupiga sehemu hiyo siku ya Jumanne asubuhi.

Maofisa wa serikali wanasema wanatarajia kuhamisha zaidi ya watu nusu mulioni.

Kimbunga Mora kinatarajiwa kuleta maafa makubwa huku maafisa wakitaka juhudi zaidi kufanyika ikiwemo kuongeza boti za uokoaji.

Shughuli nyingi muhimu katika maeneo hayo zimesimamishwa.