Polisi watoa picha mpya za mlipuaji wa Manchester

Abedi akiwa na sanduku lake la nguo
Image caption Abedi akiwa na sanduku lake la nguo

Polisi wa Uingereza wanaochunguza mlipuko wa Manchester wametoa taswira mpya kuhusu mshambuliaji, Salman Abedi, aliyebeba sanduku la nguo la rangi ya bluu.

Wanafanya uchunguzi ili kupata taarifa zake na kujua mizunguko yake ya siku nne nyuma kabla ya shambulizi, na wanaamini ni mmiliki wa sanduku la hilo la nguo.

Mlipuko waua 19 Manchester

Picha za aliyefanya shambulizi Manchester zatolewa

BBC pia imepata picha za CCTV zikimuonyesha Abedi akinunua chakula na kusafisha mazingira, siku moja kabla ya shambulizi.

Wanaume kumi na nne wako chini ya ulinzi wakihusishwa na shambulio hilo lililotokea wiki iliyopita.