Theresa May: Niko tiyari kujitoa mazungumzo ya Brexit

Theresa May aliingia madarakani mwaka 2016 baada ya aliyekuwa waziri mkuu David Cameron kujiuzulu kwa kushindwa kuzuia kujitoa kwenye umoja wa Ulaya
Image caption Theresa May aliingia madarakani mwaka 2016 baada ya aliyekuwa waziri mkuu David Cameron kujiuzulu kwa kushindwa kuzuia kujitoa kwenye umoja wa Ulaya

Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May amesema kuwa yupo tayari kutoka nje na kuachana na mazungumzo kuhusiana na kujitoa katika jumuiya ya Ulaya, iwapo tu kutakuwa na makubaliano mabaya.

Mahojiano yake yalirushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya Sky News, na Channel Four.

Bi Theresa May alisisitiza kuwa watakuwa pale kujadiliana makubaliano mazuri, na kusema kuwa ni bora kutokuwa na makubaliano, kuliko kuwa na makubaliano mabaya.

Corbyn alikabiliwa na maswali magumu kuhusiana na uhusiano wake wa zamani na makundi ya wapiganaji ya Ireland na mashariki ya kati.

Alikosolewa pia kutokana na kuhudhuria tukio la wanachama wa IRA mwaka 1987

Uingereza inatakiwa kujitoa kutoka jumuiya ya Ulaya ndani ya miaka miwili kwa mjibu wa utaratibu.