Kiongozi wa zamani wa Panama Manuel Noriega afariki

Aliyekuwa Jenerali wa Panama Manuel Noriega yuko katika hali mahututi
Image caption Aliyekuwa Jenerali wa Panama Manuel Noriega alikuwa katika hali mahututi tangu Machi

Jenerali Manuel Antonio Noriega, kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Panama, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, maafisa wametangaza.

Noriega alifanyiwa upasuaji hivi majuzi baada ya kuanza kuvuja damu kufuatia upasuaji kwenye ubongo wake.

Noriega awali alikuwa mshirika mkuu wa Marekani lakini aliondolewa madarakani kwa nguvu wanajeshi wa Marekani walipovamia nchi yake mwaka 1989.

Baadaye, alifungwa jela Marekani baada ya kupatikana na makosa ya ulanguzi wa madawa ya kulevya na utakatishaji wa pesa.

Alipatikana pia na makosa Ufaransa, na kisha Panama, ya mauaji, ufisadi na wizi wa mali ya umma.

Alikuwa ameachiliwa huru kutoka gerezani Januari kumruhusu kufanyiwa upasuaji kwenye ubongo wake.

Kifo chake kimetangazwa na Waziri wa Mawasiliano wa Panama Manuel Dominguez.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dikteta wa zamani wa Panama Manuel Noriega kwenye picha iliyopigwa 2011

Mada zinazohusiana