Jeshi la Ufilipino lapiga hatua Marawi

Wanajeshi maalum wa Ufilipino wanakabiliana na wanamgambo wa Kiislamu Marawi 29 Mei 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi maalum wa Ufilipino wanakabiliana na wanamgambo wa Kiislamu Marawi

Jeshi la Ufilipino limesema limepiga hatua kubwa katika kuukomboa mji wa Marawi kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu, huku makabiliano yaliyosababisha vifo vya watu 100 yakiendelea.

Jeshi hilo limesema wanamgambo hao kwa sasa wanadhibiti maeneo machache sana ya mji huo wa kusini mwa Ufilipino.

Bado kuna taarifa za mapigano kuendelea na maelfu ya raia wamekwama katika mji huo.

Raia 19 wamethibirishwa kufariki, baadhi wakipatikana kwenye korongo wakiwa na majeraha ya risasi vichwani.

Wapiganaji wanaoegemea kundi la Islamic State waliingia katika barabara za mji wa Marawi na kuanza mapigano baada ya jeshi kujaribu kumkamata mmoja wa viongozi wakuu wa kundi hilo.

Wengi wa wakazi walitoroka baada ya vita kuzuka, lakini afisa mmoja wa serikali anasema kuna watu 2,000 ambao hawakufanikiwa kutoroka maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji hao.

Msemaji wa Majeshi ya Ufilipino Brigidia Jenerali Restituto Padilla alsiema wanajeshi "wanaudhibiti mji wote ila maeneo machache sana" ambayo bado yanadhibitiwa na kundi la Maute.

Alisema kuna wapiganaji kati ya 40 na 50 waliosalia katika mji huo, lakini hawa huenda wakaongezeka baada ya wapiganaji kuachilia wafungwa karibu 100 kutoka kwenye jela moja.

Jenerali Padilla alsiema wanajeshi 18 wameuawa na zaidi ya wapiganaji 61 wa Maute kuuawa kwenye mapigano hayo.

Taarifa zinasema wapiganaji hao bado wanashikilia mateka watu kadha, akiwemo kasisi na Wakristo kadha.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanamgambo wa Maute waliweka bendera nyeusi sawa na za IS katika maeneo ya mji huo

Raia wengi wa Ufilipino ni Wakristo, lakini maeneo ya Waislamu, hasa Mindanao yamekuwa yakipigania kujitenga.

Mji wa Marawi hufahamika kama 'Jiji la Kiislamu' nchini Ufilipino kutokana na idadi kubwa ya Waislamu huko.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii