Wauawa kwa bomu wakila aiskrimu, Iraq

Mgahawa wa aiskrimu ulioshambuliwa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgahawa wa aiskrimu ulioshambuliwa

Watu 10 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kulipuka nje ya mgahawa wa kuuzia aiskrimu.

Shambulio hilo limetokea wakati wa jioni baada ya watu wakiwa wanaendelea kula futari, katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

Eneo hilo linakaliwa na watu wengi wa madhehebu ya Shia, huku habari zikisema kuwa ndio walikuwa walengwa.

Kufuatia shambulio hilo mjumbe wa Marekani katika kikosi cha Muungano wa majeshi yanayopambana na kundi la Islamic State Brett McGurk amelaani shambulio hilo lililotokea jana usiku.

Amesema shambulio hilo lililofanywa na IS ni baya kutokana na kulenga watoto na familia zao ambao walikuwa wakiburudika kwa kula aiskrimu wakati wa jioni baada ya mfungo wa Ramadhan.

Mada zinazohusiana