Ugonjwa wa kutopenda kula na Ramadhan

Changamoto zinazomkuta Habiba katika mwezi wa Ramadhan
Image caption Changamoto zinazomkuta Habiba katika mwezi wa Ramadhan

Wakati Ramadhan ikiwa imeanza siku chache zilizopita, kwa waislamu kujizuia kula mchana.

Mfungo huu mtukufu wa Ramadhan, umekuwa na changamoto kwa wengine.

Habiba Khanom mwenye umri wa miaka 24 ni miongoni mwao, ni mmoja wa Waislamu wachache ambaye amezungumza wazi kuhusiana na matatizo yake ya kula.

Aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, wakati akiwa bado msichana mdogo.

''..Kila mwaka, mfungo wa Ramadhan unapoanza, nakabiliwa na maamuzi magumu...'' alisema Habiba

Hata hivyo anasema huo si uamuzi wake, bali ni wa Matabibu, juu ya kama anaweza kufunga Ramadhan ama la.

Image caption Habiba anakabiliwa na matatizo ya kutokupenda kula

Katika mazingira ya kawaida, Habiba anakiri kwamba angependa kufunga, lakini anasema itakuwa kwa malengo mengine, kwa sababu atakuwa anazingatia zaidi kupunguza unene kuliko umuhimu wa dini.

''..Mwaka huu, najihisi siko tayari, bado nafuatilia ushauri wa madaktari wa kutokufunga Ramadhan...'' alisisitiza Habiba

Anasema katika miezi kadhaa iliyopita , alikuwa akiendelea vizuri katika kurudia hali yake ya kawaida, huku akipambana kuondoa mawazo, ili asijitese na njaa.

Habiba anasema katika kipindi chote hiki cha Ramadhan, anajihisi wivu kwa wenzake kuweza kufunga Ramadhan na hivyo ina maana ya kwamba yeye anazidi kutengwa na familia yake na marafiki zake.

Image caption tende na ulaji mwingine wakati wa Ramadhan

Anaona chakula kimekuwa kikitawala zaidi katika mfungo wa ramadhan, kwa wengi kuzungumzia ftari (mlo wa jioni baada ya kufunga)

Habiba amekuwa akitumia mitandao ya kijamii, kuelezea matatizo yake ya kutopenda kula na kusema ingawa bado hajakutana na muislamu yoyote, ambaye anazungumzia changamoto katika mwezi wa Ramadhan, lakini katika mtandao wa Twitter amekutana na baadhi yao.