Antonio Guterres aonya juu ya tishio la mabadiliko ya tabia nchi

Guterres amesema ni muhimu dunia kuwa sehemu salama ya kuishi
Image caption Guterres amesema ni muhimu dunia kuwa sehemu salama ya kuishi

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema ni muhimu kwa nchi zote duniani kusimia kidete utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na tishio la mabadiliko ya tabia nchi.

Akiongea katika chuo cha New York, Guterres amesema dunia ipo katika hatari na kama nchi hazitafanyia kazi makubaliano ya mkutano wa Paris juu ya tabia nchi, hali itakuwa mbaya zaidi.

Hakumtaja Rais Donald Trump ambaye hivi karibuni alikataa kuungana na viongozi wengine wa G7 katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Trump alisema atatoa msimamo wa Marekani juu ya suala hilo wiki hii.