Afungiwa kushiriki French Open kwa kumbusu mwandishi wa habari

Tukio hilo lilitokea baada ya Hamou kuchapwa na Pablo Cuevas wa Uruguay
Image caption Tukio hilo lilitokea baada ya Hamou kuchapwa na Pablo Cuevas wa Uruguay

Mchezaji wa Tenisi Maxime Hamou amefungiwa kushiriki michuano ya French Open mjini Paris, baada ya kujaribu kumbusu mwandishi wa habari mara kadhaa wakati wa mahojiano.

Mfaransa huyo mwenye miaka 21 alijaribu kumbusu Maly Thomas huku akiwa amemshika mabega yake na shingo licha ya mwanadada huyo kukataa mara kwa mara.

Image caption Hamou katikati akiwa ameinama kumbusu Maly Thomas

Alikuwa akihojiwa siku ya jumatatu baada ya kupoteza mchezo wake katika mzunguko wa kwanza.

Katika taarifa yake, chama cha Tenisi nchini Ufaransa kimesema kitendo hicho ni cha kukemewa kwa nguvu.