Temer apewa saa 24 kuijibu polisi tuhuma za rushwa zinazomkabili

Temer aliingia madarakani mwaka 2016
Image caption Temer aliingia madarakani mwaka 2016

Mahakama kuu nchini Brazil imetoa saa 24 kwa Rais wa nchi hiyo Michel Temer kuijibu polisi juu ya maswali muhimu yahusuyo yeye kuhusika katika rushwa ,jambo linalotishia maisha yake ya siasa.

Tuhuma hizo zinahusisha kampuni kubwa ya usindikaji nyama ,JBS, kuwa Temer alipokea kiasi kikubwa cha fedha kama rushwa.

Temer amepinga tuhuma hizo na kusema kuwa hatojiuzulu.

Tiyari baadhi ya vyama vya siasa vimejiondoa katika muunganiko wa serikali ya Temer.