Jopo la bunge laomba kumchunguza wakili wa Trump

Michael Cohen ni wakili wa rais Donald Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michael Cohen ni wakili wa rais Donald Trump

Wakili wa rais Donald Trump amepata maombi ya kutoa habari kutoka kwa majopo mawili ya bunge la Congress yanayochunguza muingiio wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Michael Cohen alithibitisha kwa vyombo vya habari vya Marekani kwamba alitakiwa kutoa habari na ushahidi kuhusu mawasiliano yoyote aliyokuwa nayo na Kremlin.

Bwana Cohen alisema kuwa alikataa ombi hilo kwa kuwa liliangazia maswala mengi ambayo hakuweza kujibu.

Wiki iliopita mkwe wa rais Trump Jared Kushner alitajwa katika uchunguzi huo wa Urusi.

Bwana Cohen ndio mshirika wa karibu wa Trump kukataa kuhusishwa na uchunguzi huo wa bunge la Congress na lile la Seneti kuhusu swala hilo.

''Nilikataa mwaliko huo kushiriki kwa kuwa wito wenyewe ulikuwa umeangaziwa vibaya, ukigusia maswala mengi ambayo sina uwezo kujibu'', aliambia chombo cha habari cha ABC.

Mkwe wake anadaiwa kuchunguzwa katika uchunguzi huo wa FBI.

Image caption Mkwe wa rais Trump Jared Kushner

Kulingana na chombo kimoja cha habari bwana Kushner ambaye ni mshauri mkubwa wa ikulu ya Whitehouse alitaka kufanya mawasiliano ya siri na balozi wa Urusi nchini Marekani wakati walipokutana mwezi Disemba.

Katika mkutano na vyombo vya habari, katibu wa maswala ya wanahabari Sean Spicer alikataa kuhusishwa na swala la iwapo bwana Kushner alijaribu kufanya mawasiliano ya siri.

Spicer alisema kuwa madai hayo yanatokana na ripoti ambayo haikuthibitishwa na chochote isipokuwa duru zisizojulikana.

Aliambia CNN kwamba wabunge hao hawajatoa ushahidi wowote ambao ungethibtisha kuwepo na mwingilio huo wa Urusi.

Kupanuka kwa uchunguzi huo unaodai kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani unatishia kuuzonga utawala wa rais Trump.